Kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake Stephane Dujarric, Guterres amesema "ana wasiwasi mkubwa kutokana na mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Marekani katika kipindi cha kati ya tarehe 17 na 18 Aprili ndani na karibu na bandari ya Ra's Isa ya Yemen, ambayo yameripotiwa kusababisha vifo vya raia kadhaa, ikiwa ni pamoja na wafanyakazi watano wa huduma za kibinadamu waliojeruhiwa".
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa kauli hiyo baada ya mashambulizi ya anga ya Marekani yaliyolenga bandari katika mkoa wa Al Hudaydah nchini Yemen mwishoni mwa Alkhamisi kuripotiwa kuua takriban watu 74, wakiwemo wafanyakazi watano wa sekta ya afya.
Kupitia taarifa yake hiyo, Guterres ameeleza pia "kushtushwa" na ripoti za uharibifu mkubwa wa miundombinu ya bandari na uwezekano wa uvujaji wa mafuta kwenye Bahari Nyekundu.
Kufuatia mashambulizi ya kinyama yaliyofanywa Alkhamisi usiku na ndege za kivita za Marekani katika bandari ya Ra's Isa, serikali ya Yemen imetoa taarifa ikiapa kuwa, uhalifu huo hautapita bila kujibiwa na kusisitiza kwamba Washington haitaambulia chochote ila kushindwa na kufeli kwa fedheha. Jeshi la Marekani limedai kuwa bandari hiyo ni chanzo cha mafuta kwa Harakati ya Muqawama ya Ansarullah.
Majimbo ya Sana'a, al-Bayda na Hudaydah pia yalikumbwa na mashambulizi hayo. Marekani imezidisha mashambulizi yake mabaya dhidi ya nchi hiyo maskini tangu mwezi uliopita, kwa amri ya moja kwa moja ya Rais wa nchi hiyo Donald Trump.../
342/
Your Comment